LIGI YA ENEO BUNGE LA MALINDI YAANZA RASMI

Ligi ya eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi kwenye msimu mpya wa 2022/2023 ilianza rasmi wikendi hii na mechi vijana wa Goshi katika uwanja wao wa nyumbani walishushiwa kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Real Malindi.

Mabao mawili ya Omara Bahola katika dakika ya 30 na ya tisa mtawalia ndiyo yaliyotosha kuwapa ushindi wa mechi ya ufunguzi vijana hao wa Malindi.

Matokeo mengine ya mechi za ufunguzi ni kwamba Kathama walipiga sare ya 1-1 dhidi ya Arrowhead fc wakati Black Hunters wakisajili ushindi wa bao 1-0 dhidi ya shakahola katika uwanja wao wa nyumbani na Bombi wakaitandika Lango Baya kichapo cha mabao 3-0.

Kulingana na mwenyekiti ya fkf eneo bunge la Malindi bwana Tom Langoni kwamba mashindano haya yamechanganywa katika eneo lote tofauti na awali ambapo yalikuwa yamegawanywa kimaeneo.

Tom anasema kwamba vilabu vimepungua katika ligi hiyo hii ikitokana na ukata wa kifedha za usajili pamoja na hofu ya kukosa hela za kuendesha ligi.