Afisa wa dharura katika shirika la kutetea haki za kibinadam la MUHURI Francis Auma, amelalamikia hatua ya serikali kuwahangaisha baadhi ya wanaharakati wanaofanya maandamano humu nchini akisema sio sahihi.
Kulingana na Auma ni kuwa hatua ya wanaharakati kuandaa maandamano kutokana na kuwepo kwa gharama ya juu ya vyakula, ni haki yao kwa mujibu wa sheria na wala serikali haipaswi kuwakamata wanapoendeleza shughuli hiyo.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, mwanaharakati huyo amesema kuwa suala hilo ni njia mojawapa ya kuwandamiza wakenya, kutozungumzia hali ngumu za kiuchumi wanazopia, ambazo anadai zimechangiwa pakubwa na serikali.
Aidha, amekashifu vikali kisa cha mcheshi na muigizaji Eric Omondi, kukamatwa na maafisa wa polisi kwa mara ya pili katika kaunti ya Nairobi, wakati alipokuwa akiendeleza maandamano ya amani na pia alipokuwa akidai kuwagawia wakenya unga kaunti hiyo.
FRANCIS AUMA AILAUMU SERIKALI KWA KUWAHANGAISHA WANAHARAKATI WANAOANDAA MAANDAMANO NCHINI

