Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Mombasa, Martin Kivuva ameitaka jamii kaunti ya Mombasa na Pwani kwa jumla, kushirikiana katika kuhakikisha kuwa usalama unadumishwa katika jamii.
Akizungumza na wanahabari katika kaunti ya Mombasa, kiongozi huyo wadini amesema kuwa licha ya jukumu la usalama kupewa maafisa wa polisi, jamii pia inapaswa kushirikiana katika kuwafichua wahalifu wanaotatiza amani ya wananchi.
Amesema kuwa ipo haja ya wanajamii kuzungumza na baadhi ya vijana wanaokisiwa kuwa wahalifu, kuacha kutekeleza visa hivyo kwani sio sahihi na pia vinahatarisha maisha ya wananchi.
Vile vile amesema kuwa ipo haja ya serikali kuwasaidia wananchi kumudu gharama ya maisha, kwani ukosefu wa mahitaji muhimu kutokana na mfumuko wa bei ya bidhaa sokoni, ndiyo chanzo cha kuwepo kwa mizozo ya kifamiliana na hata ukosefu wa usalama katika mitaa mbali mbali ya taifa hili.
ASKOFU MARTIN KIVUVA AITAKA JAMII KAUNTI YA MOMBASA NA PWANI KWA JUMLA KUSHIRIKIANA

