Afisa wa dharura katika shirika la kutetea haki za kibindamu la MUHURI kaunti ya Mombasa Francis Auma amesema kuna ongezeko la visa vya uhalifu hasa katikati mwa mji huo wa Mombasa.
Kulingana na Auma maeneo ya Mwembe Tayari, barabara ya Nkrumah, barabara ya Moi na maeneo ya Posta kuwa miongoni mwa yale ambayo yamejaa visa vya uhalifu.
Auma, amesema wezi wanaowahangaisha wenyeji wanaoendeleza shughuli zao katikati mwa mji huo hutumia pikipikia katika kutekeleza visa hivyo.
Aidha, ametoa wito kwa asasi za usalama kuweka mikakati thabiti ya kuwakabili wahalifu hao ili kuimarisha usalama katika kaunti ya Mombasa.
MUHURI YATOA WITO KWA ASASI ZA USALAMA KUKABILI VISA VYA UHALIFU KAUNTI YA MOMBASA

