Mahakama kuu ya Malindi kaunti ya Kilifi imebatilisha ushindi wa mbunge wa Magarini Harrison Gharama Kombe.
Akitoa uamuzi huwo jaji wa mahakama hiyo Alfred Mabeya, amesema uchaguzi wa wadhifa wa ubunge eneo Hilo la Magarini, ulikumbwa na udanganyifu mwingi wakati wa kuhesabiwa kwa kura na hata kabla ya kutangazwa kwa ushindi wa Kombe.
Aidha, Mahakama hiyo imeiagiza tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC kaunti ya Kilifi, kuandaa upya uchaguzi wa ubunge eneo hilo la Magarini kwa mujibu wa sheria.
Katika uchaguzi huo, Harrison Kombe alipata jumla ya kura 11,946 huku Stanley Kombe akipata kura 11,925 na aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Micheal Kingi akipata kura 7,921.
Ikumbukwe kwamba Stanley Kenga kupitia chama cha UDA na Micheal Kingi wa chama cha PAA, ndio waliowasilisha kesi hiyo mahakamani kupinga ushindi wa Harrison Kombe ambaye aliwania wadhifa huo akitumia chama cha ODM.
MAHAKAMA YA MALINDI YABATILISHA USHINDI WA MBUNGE WA MAGARINI

