Mkufunzi wa ligi ya daraja la pili kitaifa Peter Ponda anayekiongoza kikosi cha Beach Bay anasema sababu kubwa ya kufanya klabu hiyo kuandikisha matokeo duni msimu huu ni kutokana na baadhi ya wachezaji tegemezi kujiondoa kikosini hapo.
Baadhi wa wachezaji anaowakosa ni pamoja na Amani Kiponda aliyehamia klabu ya Mombasa Omax FC ambayo pia yacheza daraja la pili huku Erick Japheth lakini pia Kasena Sulubu wakiondoka klabuni hapo kutokana na masuala ya kikazi.
Katika mechi mbili zilizopita klabu hiyo ya mjanaheri imesajili alama nne na kupanda hadi nafasi ya 12 wakiwa na alama 10 mpaka kufikia sasa.

