Liverpool inayoongozwa na mkufunzi Jergen Klopp usiku wa kuamkia leo imesajili ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wolveshampton katika uwanja wao wa nyumbani Anfield.
Bao la Virgil Van Dijk katika dakika ya 73 kupitia assist ya Diogo Jota na bao la Mohamed Salah katika dakika ya 77 ndio mabao yalotosha kuwapa ushindi majogoo hao wa Mersyside.
Mechi nyingine wa ligi kuu uingereza iliyochezwa usiku wa kuamkia leo ni ile ya Arsenal ambao wamesajili ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya klabu ya Everton.

