Usiku wa leo kuna mechi ya Elclassico ambapo Real Madrid watakuwa wanafufua uhasama wao dhidi ya klabu ya Barcelona katika mtanangwe wa Copa Del Rey hatua ya nusu fainali raundi ya kwanza.
Mechi hiyo itakayochezwa dimbani Santiago Barnabou itamkosa mshambuliaji Robert Lewandoski ambaye anauguza jeraha la misuli pamoja na Osuamnane Dembele pamoja na kiungo wa Uhispania Pedri.
Kwa upande wa Real Madrid David Alaba pamoja na Ferland Mendy watakosekana katika kikosi hicho cha mkufunzi Carlo Ancelotti.
Mechi hiyo itakuwa inarindimwa usiku wa saa tano hii leo saa za Afrika Mashariki.

