UMOJA WETU NDIO NGUVU YETU MSIMU HUU

Mkufunzi wa klabu ya Samburu Lions Alex Badizo anasema kwamba umoja wa wachezaji wake pamoja na motisha wao katika mazoezi ndio jambo linalochangia klabu hiyo kuandikisha matokeo mazuri msimu huu katika ligi ya daraja la pili kitaifa.

Simba hao wa samburu kutoka kaunti yak wale wamesajili alama 11 kati ya 15 kwenye mechi tano zilizopita kwa kushinda mechi tatu na kutoa sare mbili.

Samburu Lions inasimama katika nafasi ya tatu ligini wakiwa na pengo la alama tano nyuma ya viongozi wa ligi Omax FC kutoka kaunti ya Mombasa.