WENYEJI WA KAUNTI YA LAMU WAPATA IDHINI YA KUHIFADHI NA KULINDA MIKOKO

Wakaazi wa Lamu wamepata idhini ya kuhifadhi na kulinda mikoko baada ya mkataba wa maelewano kuwekwa kati yao, serikali na mashirika mbalimbali ya kuhifadhi mikoko.
Ni hatua ambayo inalenga kuimarisha mikoko na kuboresha kiuchumi kaunti hiyo ya Lamu na hii kutokana na asilimia 60 ya mikoko yote humu nchini kupatikana kaunti hiyo ya Lamu.
Aidha zaidi ya wakaazi elfu 30 katika kaunti ya Lamu wanategemea mikoko kujikimu kiuchumi.
Mkataba huo unalenga kuhakikisha wenyeji wanapata fursa ya kunufaika kupitia raslimali hiyo pasipo vikwazo vyovyote.
Wakati huohuo, akina mama katika kaunti hiyo wamehimizwa kuhakikisha kuwa wanashiriki pakubwa katika uhifadhi na utunzaji wa mikoko katika maeneo yao