Maafisa wa tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC kanda ya pwani kaskasini wakishirikiana na maafisa wa polisi wamefaulu kumtia mbaroni afisa mmoja wa kaunti ya Tana River katika uwanja wa ndege wa Malindi kaunti ya Kilifi akiwa na shilingi milioni mbili na laki saba.
Akithibitisha kukamatwa kwa afisa huyo meneja wa tume hiyo Hassan Khalid amesema afisa huyo kwa jina Mariam Abdalla alikua tayari ameabiri ndege na akakamatwa na maafisa wa polisi wa uwanja wa ndege wa Malindi.
Aidha Meneja huyo amesema afisa huyo ni mfanyikazi wa kaunti ya Tana River kutoka idara ya fedha na haijabainika kiini cha afisa huyo kusafiri kwa ndege akiwa na kima hicho cha pesa taslim japo maafisa hao wameanzisha uchunguzi wa kina.
Kwa upande wake wakili wa afisa huyo Morris Kilonzo amethibitisha mteja wake kukamatwa katika uwanja wa ndege wa Malindi na kwamba kwa sasa wanafuatilia huku wakiwa wanaendelea kuandikisha taarifa ya umiliki wa fedha hizo.
MAAFISA WA EACC KANDA YA PWANI KASKAZINI WAMTIA MBARONI AFISA ANAYEFANYA KAZI KATIKA SERIKALI YA KAUNTI YA TANA RIVER

