Wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta hususan wanaoishi karibu na mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Tsavo wanalalamikia kero la wanyamapori na kulitaka shirika Hilo kuwajibika ipasavyo.
Wakiongozwa na mwakilishi wa wadi ya Wumingu – Kishushe Newton Kifuso wanasema uvamizi huo unasababisha shughuli zao nyingi kulemazwa.
Aidha, Kifuso ametoa wito kwa idara ya usalama kushirikiana na maafisa wa KWS ili kushika doria katika maeneo yaliyoathirka.
Kifuso ametaja maeneo ya Paranga, Sechu, Mlilo, Kasigau, miongoni mwa mengineyo kama maeneo yaliyoathirika zaidi hali inayosababisha wakaazi kuishi wakitegemea chakula cha msaada baada ya mimea Yao kuharibiwa na wanyamapori.
WENYEJI WA TAITA TAVETA WANAOISHI KARIBU NA MBUGA YA WANYAMAPORI YA TSAVO WAIBUA LALAMA ZAO

