Rais William Samoei Ruto ameahidi kulishughulikia suala tata la ardhi katika kaunti ya Lamu ili kudhibiti mizozo inayotokana na umiliki ardhi kwenye kaunti ya Lamu.
Akizungumza jana katika uwanja wa muungano eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu Rais Ruto amesema atafanikisha ahadi ambazo alitoa wakati wa kampeni za uchaguzi kuhusu suala tata la ardhi kwenye kaunti hiyo.
Amesema mikakati imewekwa katika kuhakikisha mizozo hiyo inapata mwafaka.
Kwa upande wake Rigathi Gachagua ambaye ni naibu wa rais amemtaka kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga kutowapotosha wakenya akidai Raila ni miongoni mwa viongozi ambao wamechangia kwa taifa la Kenya kukabiliwa na changamoto za kiuchumi, Naye Gavana wa kaunti ya Lamu Issah Timamy amemsihi rais William Samoei Ruto kuongeza walimu katika kaunti hiyo ili viwango vya elimu viimarike hata zaidi.
Wakati huohuo mbunge wa Lamu Mashariki Ruweida Obo amemtaka Rais Ruto kuboresha barabara za eneo bunge hilo naye Seneta wa kaunti hiyo Joseph Guthuku akitaka wavuvi walioathirika na ujenzi wa bandari ya Lapsset kulipwa fidia yao.
RUTO AMEAHIDI MIZOZO YA ARDHI KUTATULIWA KAUNTI YA LAMU

