ROSTAM AZIZI ATOA WITO KWA SERIKALI ZA AFRIKA MASHARIKI KUIMARISHA UWIANO

Mwekezaji na pia mmiliki wa Gesi kutoka taifa la Tanzania Rostam Aziz ametoa wito kwa serikali za kanda ya Afrika Mashariki kuimarisha uwiano miongoni mwa raia wake ili kuboresha masuala ya biashara.
Kwa mujibu wa Aziz, serikali za mataifa yaliyowanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimefeli katika kuboresha mazingira bora ya kibiashara licha ya kuwa na uwezo wa kuwashirikisha wawekezaji mbalimbali wakiwemo kutoka mataifa nje.
Aidha, amemtaka rais William Samoei Ruto kuweka mikakati thabiti ambayo itasaidia kuimarisha mazingira bora ya kibiashara nchini Kenya kama mfano bora kwa mataifa mengine ya kanda ya Afrika Mashariki.
Vilevile, amewahimiza marais wa Afrika Mashariki kushirikiana na kuondoa vikwazo ambavyo vinazuia kuwepo kwa mazingira bora ya uwekezaji na kuimarika kwa biashara akisema iwapo hilo litatiliwa maanani uchumi wa ukanda wa Afrika Masharika utaimarika kwa asilimia kubwa.