Beki wa ureno mwite Joao Cancelo amesema alishindwa kukataa ofa ya mkopo kuondoka Etihad na kujiunga na Bayern Munich kwa kile anachotaja kwamba mkufunzi wake Pep Guardiola wa Manchester City alimnyima muda zaidi wa kucheza klabuni hapo jambo ambalo lilikuwa linahatarisha kushuka kiwango chake.
kwa sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anachezea Baeyrn Munich kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu mkataba wake ukiwa na kipengele cha kununuliwa na klabu hiyo.
Klabu ya Liverpool imeonyesha nia ya kutaka kumnunua beki wa RB Leipzig pamoja na timu ya taifa ya Croatia mwite Josko Gvardiol mwenye umri wa miaka 21.
Mchezaji huyo ni mfungaji wa bao la usiku wa kuamkia leo ambapo klabu yake imepiga sare dhidi ya Manchester City katika dimba la Red Bull Arena kwenye mechi ya klabu bingwa ulaya.

