Waziri wa madini na uchumi wa raslimali za baharini nchini Salim Mvurya amesema mwekezaji ambaye anachimba madini katika eneo la Kishushe, Wundanyi kaunti ya Taita Taveta ameahidi kulipa wenyeji jumla ya shilingi milioni 30 ambazo amekuwa akidaiwa na wenye ardhi kwa zaidi ya miaka 3.
Mvurya ameitaja kama hatua ambayo inaridhisha kwani awali juhudi za wenyeji kudai fedha zao zilikumbwa na changamoto.
Mvurya amesema wamekubaliana na mwekezaji huyo kuanza kuwalipa wenyeji hao kuanzia wiki ijayo.
Haya yanajiru huku wamiliki wa shamba ambapo uchimbaji wa mdini unatekelezwa wakisema ni afueni kwao kwani wamedai fedha hizo kwa muda mrefu bila mafanikio.
MWEKEZAJI ANAYECHIMBA MADINI ENEO LA KISHUSHE AMEAHIDI KULIPA WENYE ARDHI FEDHA ZAO

