Gavana wa kaunti ya Kilifi Gedion Maitha Mung’aro amesema wanapania kuongeza mgao wa fedha za basari kwa wanafunzi ili kuwawezesha wale ambao walipata alama za juu wanajiunga na shule za upili kwa wakati ufaao.
Amesema serikali ya kaunti ya Kilifi inapania kutenga kima cha shilingi bilioni moja ili kufanikisha hilo.
Awali serikali ya kaunti ya Kilifi ilikuwa imetenga shilingi milioni 350 ili kufadhili elimu kwa wanafunzi wa kaunti ya Kilifi japo fedha hizo zimekuwa hazitoshi ikilinganishwa na idadi kubwa ya wanafunzi ambao wanajiunga na shule za upili kaunti ya Kilifi.
Vilevile, amesema wanafunzi wengi katika kaunti ya Kilifi wamekuwa wakilazimika kutafuta ufadhili kutoka wa wahisani mbalimbali ili kujiunga na shule za upili kutokana na uchache wa fedha hizo kwa serikali ya kaunti ya Kilifi.
GAVANA WA KAUNTI YA KILIFI GEDION MUNG’ARO ASEMA WANAPANIA KUONGEZA MGAO WA FEDHA ZA BASARI

