Baraza la dini mbalimbali la Amani na maridhiano kutoka taifa la Tanzania limetoa wito kwa wafuasi wa dini ya Kiislami nchini kusitisha migawanyiko miongoni mwao ili kuwe na umoja.
Kulingana na mwenyekiti wa baraza hilo nchini Tanzania Sheikh Alhad Musa Salaam ambaye alikuwa akizungumza kwenye kongamano la viongozi wa dini hilo ambalo limeandaliwa na baraza la mashauri ya Kiislamu nchini KEMNAC katika kaunti ya Mombasa, amesema ni jambo la kusikitisha kuona Waislamu nchini Kenya wakizozana hali ambayo inaendelea kuwatenganisha wafuasi wa dini hiyo.
Amesema ili kuwe na umoja pamoja na amani ni lazima kuwe na ushirikiano mzuri baina ya waumini wa dini hiyo.
Aidha, Sheikh Salaam amewahimiza Waislamu kuhakikisha wanadumisha amani kwa jamii na kujiepusha na mizozo baina yao.
Naye Sheikh Juma Ngao ambaye ni mwenyekiti wa baraza la KEMNAC amewataka Waumini wa dini ya Kislamu nchini kujitenga na Mabishani pamoja na chuki akisema inaregesha nyuma Masuala mbalimbali yanayohusiana na dini hiyo.
DINI YA WAUMINI WA KIISLAMU WAHIMIZWA KUWA NA UMOJA

