Sipika wa bunge la kaunti ya Lamu Azhar Ali Mbarak amepuzilia mbali madai ambayo yamekuwa yakiibuliwa dhidi yake kuwa aliwania wadhifa huo wa Uspika ili kuhujumu harakazi za uongozi wa kaunti hiyo katika kufanikisha maendeleo kwa wenyeji.
Akipinga madai hayo amesema lengo lake kuu la kuwania wadhifa huo ni kuhakikisha wenyeji wa kaunti ya Lamu wanahudumiwa vilivyo mkwa mujibu wa katiba ya nchi na wala sio kuhujumu utendakazi wa serikali ya kaunti hiyo kupitia misuada inayowasilishwa bungeni.
Kwa mujibuwa Azhar hakuna msukumo wa ufadhili ambao alipata kutoka kwa baadhi ya watu wenye ushawishi mkubwa kwenye serikali ya kaunti ya Lamu ambao wanapania kumtumia kama kibaraka kwa manufaa yao Wenyewe.
Hatahivyo Mbarak ameishinikiza serikali ya kaunti ya Lamu kuwapa nafasi sawa za uakilishi jamii ya wafugaji wanaoishi Lamu ikiwemo nafazi za uaziri na kusema hakuna hata mtu mmoja kutoka jamii ya wafugaji ikilinganishwa na jamii zengine katika kaunti ya lamu ambaye ameajiri.
SPIKA WA BUNGE LA KAUNTI YA LAMU APINGA MADAI AMBAYO YAMEKUWA YAKIIBULIWA DHIDI YAKE

