Idara ya usalama katika kaunti ya Tana River imetakiwa kutumia njia ya mazungumzo katika kuleta suluhu la mizozo, iliyoko katika kaunti hiyo na kupata suluhu la kudumu.
Kwa mujibu wa gavana wa kaunti hiyo Dhado Godana zipo njia nyingi za wananchi kusuluhisha matatizo yanayowakabili, kando na kuwakamata vijana wanaokisiwa kuhusika katika vita kwenye jamii.
Akizungumza na wanajamii katika kaunti hiyo, amewataka wazee wa jamii zilizoathirika na ugomvi kuzungumza na vijana na kupata chanzo cha mizozo hiyo.
Vilevile, amesema tayari wameanza mazungumzo na viongozi wa kaunti jirani ya Kitui ili kupata suluhu la vita ambavyo zimekuwa vikishuhudiwa katika mpaka wa kaunti ya Tana River na Kitui.
IDARA YA USALAMA KAUNTI YA TANA RIVER YATAKIWA KUTUMIA NJIA YA MAZUNGUMZO KUSULUHISHA MIZOZO

