SERIKALI YA KAUNTI YA LAMU KUENDELEZA SHUGHULI ZA KUPANGA MIJI YA KAUNTI HIYO

Gavana wa kaunti ya Lamu, Issaa Timamy amesema wanaendeleza shughuli za kupanga upya miji ya kaunti ya Kaunti ya Lamu.
Kiongozi huyo amesema kwa sasa wapo maafisa ambao wanazunguka mashinani, ili kufanya vikao vya wananchi kutoa maoni yao kuhusiana na mipangilio ya serikali ya kaunti hiyo.
Gavana huyo amesema kuwa mji wa lamu utakuwa na sehumu mbalimbali ikiwemo afisi za kaunti na hata sehemu za burudani jambo ambalo amesema litaboresha mji huo na kaunti yote kwa jumla.
Vilevile, Timamy amesema serikali ya kaunti ya Lamu itajenga hospitali itakayokuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 50 katika eneo la Hindi.