Kwenye ligi kuu nchini uingereza sasa kumekucha baada ya klabu ya Arsenal kubimbindwa na mabingwa watetezi Manchester City katika dimba la ugenini Etihad kipigo cha mabao 3-1.
Mabao ya Manchester City yamefungwa na kiungo Kevin De Bruyne, Jack Grealish lakini pia mshambuliaji raia wa Norwey Erling Braut Halaand akashindilia ushindi huo katika dakika za lala salama. Kwa upande wa the Gunners bao la kufutia machozi limefungwa na fowadi wa timu ya taifa ya Uingereza mwite Bukayo Saka.
Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kushuka kileleni mwa ligi na kumpisha Manchester City ambaye anaongoza ligi kwa alama 51 lakini pia kwa wingi wa mabao. Ikumbukwe kwamba Arsenal ya mkufunzi Mikel Arteta bado inasalia kuwa na mechi moja kiporo.

