GAVANA WA KILIFI GEDION MUNG’ARO AWAONYA VIJANA WANAOTUMIWA VISIVYO NA WANASIASA

Gavana wa kaunti ya Kilifi, Gideon Maitha Mung’aro amewataka wananchi waliowasilisha kesi mahakamani kupinga ushindi wake baada ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka jana wa wa 2022 kutekeleza agizo la mahakama baada ya Mahakama ya Malindi kutupilia mbali hiyo.
Akizungumza nje ya afisi yake mjini Kilifi kaunti ya Kilifi, baada jaji wa mahakama hiyo ya Malindi Anne Onginjo, kuitupilia mbali kesi hiyo kwa kukosa ushahidi wa kutosha gavana huyo amewonya vijana dhidi ya kutumika na wanasiasa visivyo katika masuala ya kesi zinazohusisha uchaguzi nchini Kenya.
Ameeleza kufurahishwa na uamuzi huo na kuwapongeza mawakili waliokuwa wanawawakilisha Mahakamani, Kauli yake imeungwa mkono na naibu wake Margaret Chibule, ambaye amesema walikubali kutekeleza kila agizo lililotolewa na mahakama wakati kesi hiyo ilipokuwa ikiendelezwa kwani uongozi wao unaheshimu demokrasia ya taifa hili.
Akitoa uamuzi huo jana jaji wa mahakama hiyo ya Malindi Anne Onginjo, alisema kesi hiyo ilikosa ushahidi wa kutosha na kusababisha kuitupilia mbali.
Jaji Onginjo amewaagiza walalamishi wa kesi hiyo kulipa faini ya shilingi milioni sita kwa gavana Mung’aro, naibu wake Florence Chibule, tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC tawi la kaunti ya Kilifi pamoja na afisa mkuu wa tume hiyo kaunti ya Kilifi Hussein Gure.