VIHIGA BULLETS HALI YAO YAZIDI KUWA MBAYA LIGINI

Klabu ya Vihiga Bullets wanazidi kuonyeshwa unyonge kwenye ligi kuu ya fkf kufuatia kichapo cha jana cha mabao 3-0 dhidi ya Bidco United katika dimba lao la nyumbani mjini Mumias.

Mabao ya Bidco klabu inayotokea Thika katika kaunti ya kiambu jana yalifungwa na Henry Juma, Gaucho lakini pia goli ya kumaliza kazi kutoka kwa Ezekiel Okare kupitia mkwaju wa penalty katika dakika ya 88.

Katika dimba la Kasarani Mathare United walionyesha ufalme wao kutoka mitaa ya mabanda kwa kuwatandika Kariobangi sharks kichapo cha mabao 2-1.

Matokeo hayo sasa yanaifanya Mathare United kupanda hadi nafasi ya 16 huku Karobandi Sharks ikisalia katika nafasi 13 kwenye ligi.