Zaidi ya wakaazi elfu 20 katika kaunti ya Lamu wameathirika na baa la njaa kutokana na kiangazi cha muda mrefu kichoendelea kushuhudiwa eneo hilo kufuatia ukosefu wa mvua .
Takwimu hizi ni kutoka kwa shirika la kitaifa la kukabiliana na majanga ya ukame NDMA huku kisiwa cha Ndau, Pate na Kiwayu yakitajwa kama maeneo yalioathirika zaidi.
Aden Mohamed afisa wa NDMA amesema kuwa vijiji 14 katika maeneo hayo yatanufaika na chakula cha msaada, huku Bernad Atonga ambaye ni afisa wa shirika la WWF akisisitiza haja ya wakaazi kuimarishwa kwa kupewa mbegu wanapojitayarisha kwa msimu wa upanzi.
BAA LA NJAA LINAENDELA KUWAATHIRI WENYEJI WA LAMU

