Mkufunzi mkuu wa klabu ya Liverpool Jergen Klopp amesema kwamba fowadi wa ureno Diogo Jota, beki Virgil Van Dijk pamoja na Roberto Firmino watashirikishwa katika mechi ya usiku wa leo dhidi ya Everton katika dabi ya Merseyside itakayorindimwa katika dimba la Anfield saa tano usiku.
Mkufunzi huyo raia wa Ujerumani anasema kwamba ako tayari kuchukua jukumu la kurekebisha makosa yanayosababisha matokeo mabaya na ako na matumaini kakubwa ya kurudisha hadhi ya Liverpool licha ya kuwa na mwanzo wa msururu wa matokeo mabaya msimu huu.
Msimu huu Liverpool imesajili alama 29 baada ya mechi 20, ikisimama katika nafasi ya kumi kwa sasa fomu ambayo imeonyesha kiwango kibaya baada ya kipindi kirefu tangia mkufunzi klopp achukue hatamu ya uongozi wa klabu hiyo mwaka 2015.

