CONGO BOYS YATEUWA CHIPUKIZI 30

Klabu ya Congo Boys sasa imekamilisha kuteuwa wachezaji 30 ambao wataanza kuitumikia klabu hiyo ambayo msimu huu inajitayarisha kucheza ligi ya mkoa wa pwani.

Juma hili Congo Boys imekuwa ikifanya zoezi la kufanya majaribio ya wachezaji wa kati ya umri wa miaka 17 hadi 21 kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya wa 2022/2023.

Sasa ni rasmi klabu hiyo itacheza ligi ya mkoa kutokana na msimu uliopita kutotambulika na shirikisho la soka  la FKF ambapo Congo Boys walicheza ligi ya daraja la pili kitaifa msimu ambao ulikuwa unasimamiwa na kamati ya mpito ambayo kulingana na fkf, kamati hiyo ilikuwa haramu.