MATHARE UNITED YAMFUTA KAZI BONIFACE OMONDI

Klabu ya Mathare United imethibitisha kumfuta kazi mkufunzi Boniface Omondi kufuatia muendelezo wa matokeo mabaya tangia kuanza kwa msimu huu.

Chini ya uongozi wa Omondi Mathare United inasimama katika nafasi ya mwisho ligini na alama nne pekee wakiwa wamepoteza mechi nane, kupiga sare mara moja na kupata ushindi mara moja pekee.

Kufuatia kufutwa kwa mkufunzi huyo sasa kocha wa makipa Samuel Koko anatarajiwa kuchukua jukumu la kukiongoza kikosi hicho huku Mathare United wakitafuta mkufunzi mpya.