OMAX FC YALENGA KUINGIA DARAJA LA KWANZA MSIMU UJAO

Mkufunzi mkuu wa klabu ya Omax fc mjini Mombasa Juma Kalato anasema anamatumaini makubwa ya kupanda daraja hadi daraja la kwanza kitaifa msimu ujao.

Alikuwa akiyasema hayo baada ya kuichapa Yanga fc mjini Malindi kichapo cha mabao 4-1 katika uwanja wa Alaskan mjini malindi wikendi iliopita.

Kufikia sasa Omax imeshinda mechi zote za ligi msimu huu na wanaongoza jedwali la ligi hiyo wakiwa na alama 15 baada ya mechi tano.

Mkufunzi Kalato amesema kwamba klabu ya Omax ilifanya usajili wa kutosha kabla ya msimu mpya wa 2022/2023 kuanza rasmi na hatua iyo imewasaidia kujenga kikosi thabiti cha kung’ang’ania matokeo mazuri msimu huu.