Michezo katika kaunti ya Lamu ni kati ya silaha moja ya kupiga vita uwepo wa vita baina ya jamii zinazo zozana katika kaunti hiyo.
Hii ni kulingana na wakazi pamoja na wadau wa michezo Lamu ambao wanalalama kuwepo na ukosefu wa usalama kutokana na mashambuilizi ya magaidi wa Alshabab pamoja na jamii zinazopigana kisa ardhi na mifugo.
Kassim Farouk ambaye ni mkufunzi wa soka katika wadi ya Witu kaunti ya Lamu ametoa wito kwa serikali na viongozi kuwekeza katika mashindano ya soka ili kuwashughulisha wachezaji na hatimaye kuwaepusha na kujiingiza katika magenge ya uhalifu.
Katika siku za hivi punde kumeuwepo na taharuki inayotokana na migogoro baina ya jamii za Wapokomo na Waorma ambao wanazozania mashamba pamoja na maeneo ya kulisha mifungo.

