Mashindano ya mataifa bingwa afrika maarufu kama CHAN yamefikia katika hatua ya nusu fainali na jioni ya leo mechi mbili za kutafuta wanafainali zitakuwa zinarindimwa.
Mwendo wa saa moja usiku wa leo wenyeji wa mashindano haya Algeria watakuwa wanashuka dimbani dhidi ya Niger wakati mabingwa wa Afcon waite Senegal wakirindimana na Madagascar mwendo wa saa nne usiku.
Fainali zamashindano haya zitafanyika mwezi February, pamoja na mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne.

