GOR MAHIA YAIPIGA TALANTA, OMALA AKIZIDI KUNG’AA LIGINI

Gor Mahia ambao ni mabingwa mara 19 wa ligi kuu nchini wamesajili ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Talanta Fc katika mtanange uliochezwa dimbani Nyayo.

Benson Omala aliendelea kungaa katika mechi hiyo kwa kufunga bao lake la 10 msimu huu, huku John Macharia leo akiingiam kambani lakini pia Joshua Onyango akitikisa nyavu.

Matokeo hayo yanaifanya Gor Mahia inayoongozwa na mkufunzi Johnnathan Mckinstry kusalia na alama moja pekee kupanda kileleni mwa jedwali la ligi kuu, huku wakiwa na mechi moja kiporo.