HARAKATI ZA KUHAMISHA KICHINJIO CHA MALINDI ZINAENDELEZWA

Serikali ya kaunti ya Kilifi inaendeleza mpango wa kuhamisha sehemu ya kichinjio  mjini Malindi, kutokana na hatua ya wanajamii eneo hilo kulalamikia uharibifu wa mazingira katika sehemu hiyo.

Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi katika eneo bunge la Malindi wamepongeza hatua hiyo huku wakipendekeza sehemu hiyo, sasa kukabidhiwa rasmi wafanyabiashara wa Juakali, ili kuwapa nafasi nzuri ya kuendeleza shughuli zao na hata kuuza bidhaa wanazotengeneza.

Wakiongozwa na mwakilishi w wadi ya Shella  mjini Malindi, Twahir AbdulKarim katika mazungumzo ya kipekee na Lulu Fm ameeleza kuwa hatua hiyo ni njia mojawapo ya kuboresha shughuli za kuuboresha  mji wa Malindi.

Wakati uohuo mwakilishi wa wadi huyo amesema  ardhi ambayo inatumika na wahunzi hapa mjini Malindi, iliyo karibu na soko la Kwa jiwa, itatumiaka katika ujenzi wa maktaba ya kitaifa ambayo itasaidia wanafunzi eneo hili kuboresha masomo yake.