SERIKALI KUU YATAKIWA KUFIKISHA FEDHA ZA KUFANIKISHA MASOMO YA CBC

Mwenyekiti muungano wa walimu  KNUT tawi la kilindini kaunti ya Mombasa Ahmed Kombo Ahmed amesema kuna haja ya serikali kufikisha fedha za kufanikisha masomo ya mfumo mpya wa elimu wa umilisi CBC kwa haraka ili kuhakikisha shule zinafikia malengo.

Kombo ametaja kuwa shule nyingi za kibinafsi ndizo zilizofikia vigezo vilivyowekwa na serikali kwa mujibu wa  mfumo huo.

Wakati uo huo Ahmed ameangazia swala la wanafunzi wa kiume kuitwa shule za wasichana kwa masomo ya sekondari akisema ni sharti idara husika iingilie kati kutatua swala hilo kabla ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kufika shule zao mbalimbali walizoitwa.