WITO WATOLEWA KWA VIONGOZI KUIMARISHA MICHEZO YA KINA DADA PWANI

Viongozi wa kaunti za pwani washauriwa kuimarisha michezo ya kinadada ili kuwaepusha vijana hao kutokana na majanga mengi katika jamii yakiwemo mimba za mapema.

Wito huo umetolewa na mkufunzi wa klabu ya Malindi Progressive academy, Neema Charo ambaye amedai kwamba kijana wa kiumo kwa muda sasa amekuwa akiangaziwa katika michezo.

Mkufunzi huyo anasema kwamba viongozi wanafaa kutilia mkazo katika michezo hasa soka ambao huenda ikawa njia moja ya kijana wa kike kupata ajira na kujiendeleza jambo ambalo litakuwa limemuepusha na majanga mengi mashinani.