Mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini kenya Tusker FC wamerejea katika nafasi ya kwanza katika jedwali baada ya jana kuitandika Sofapaka kichapo cha bao 1-0 katika uwanja wa Kasarani katika jiji kuu la Nairobi.
Bao la Ibrahim Joshua katika dakika ya 26 ndilo lilotosha kuwapa ushindi vijana hao wa mkufunzi Robert Matano.
Awali mkufunzi Matano alikuwa amesema kwamba ana matumaini ya kutetea ubingwa na kikosi chake cha sasa na tayari Wanamvinyo hao wanaongoza ligi na alama 23 kwa pengo la alama moja mbele ya nafasi ya pili huku wakiwa na mechi moja kiporo.

