WACHEZAJI WAMEOLEWA, TUNATAFUTA WACHEZAJI WENGINE – JOYCE UNDA

Mkufunzi mkuu wa Kilifi Starlets Joyce Unda anasema sasa wanalenga kutafuta wachezaji wapya katika klabu hiyo ili kuchukua nafasi ya wachezaji walioondoka kujitafutia ajira na wengine kuolewa baada ya likizo ndefu msimu jana ulipotamatika.

Klabu hiyo iliyopanda daraja hadi ligi ya mkoa imekosa wachezaji wa kutosha kuchezea klabu hiyo kutokana na hali ya uchumi na hali mbaya ya maisha iliyofanya wachezaji kujiondoa uwanjani.

Licha ya changamoto nyingi kukumba klabu hiyo msimu uliopita Kilifi Starlets ilifanikiwa kuandikisha historia kwa kupanda daraja na hii kulingana na  mkufunzi Joyce Unda ni kwamba ilitokana na wachezaji wenyewe kujituma vilivyo uwanjani kutangaza vipaji vyao.