MCHUNGAJI SAMWEL MATIKO ATILIA SHAKA TAKWIMU KUTOKA SHIRIKA LA KITAIFA LA UTAFITI

Mchungaji wa kanisa la Ocean Assemblies  mjini Malindi kaunti ya Kilifi Samuel Matiko, ametilia shaka takwimu za shirika la utafiti la KENYA BUREAU OF STATISCS, kuhusiana na ongezeko la idadi ya watu wanaoshiriki ngono nje ya ndoa.

Akizungumza na mwanahabari wetu mchungaji huyo amesema kuwa licha ya kuwepo kwa visa hivyo, huenda ikawa utafiti huo ulifanyiwa watu wasiokuwa na maadili katika jamii, ambao walizingumza kile wanachohisi licha ya wao kufahamu kuwa sio ukweli.

Vile vile ametaja ukosefu wa maadili na hata suala la watu kukosa kuwa na hofu ya Mungu katika jamii, kuwa mojawapo ya mambo ambayo yamechangia pakubwa kushuhudiwa kwa ongezeko la visa vya wanandoa kuchepuka.

Aidha, amesema kuwa upo uwezekano wa wanandoa kuwa waaminifu kwa wapenzi wao huku akitoa wito kwa kanisa kujitokeza wazi na kuanza kuzungumzia masuala ya uaminifu katika ndoa kwa uwazi na undani zaidi.