Serikali ya kaunti ya Kilifi inalenga kukiboresha kiwanja cha michezo cha Water mjini Kilifi ili kuimarisha sekta ya michezo.
Kulingana wa warizi wa jinsia na michezo kaunti ya Kilifi Ruth Dama Masha kaunti ya kilifi haina viwanja ambavyo vina hadhi ya kitaifa hali ambayo inawafanya vijana wengi wanakosa nafasi ya kuinua vipaji vyao .
Waziri huyo anasema wizara yake tayari imeweka mikakati ya kuhakikisha vijana wenye talanta mbalimbali watapata nafasi ili watumie talanta zao kujipatia ajira.
Wakati huo huo waziri huyo amesema serikali ya Kilifi ina mipango ya kujenga kiwanja cha kisasa cha michezo katika chuo kikuu cha Pwani kwa kipindi hiki cha miaka mitano.

