Mbunge wa Kaloleni kaunti ya Kilifi Paul Katana ameitaka tume ya huduma za polisi nchini kuwahamisha baadhi ya maafisa wa polisi ambao wamehudumu kwa miaka mingi katika eneo bunge hilo la Kaloleni.
Kulingana na Katana uhasama ambao umekuwa ukidhiirika kati ya maafisa wa polisi na wenyeji umechangiwa na maafisa hao.
Kutokana na hilo sasa ameahidi kuwasilisha majina hayo kwa Inspekta Mkuu Jenerali wa Polisi nchini Japhet Koome ili maafisa hao wa polisi wahamishwe hadi kwenye vituo vingine vya Polisi kutokana na kile ambacho anadai wenyeji wamekuwa wakilalamikia kuhangaisha na maafisa hao wa polisi.
Vilevile, ametaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya maafisa wa polisi ambao wanajihusisha na visa vya ufisadi kwa kuchukua hongo kutoka kwa wahudumu wa pikipiki pamoja na kuwahangaisha wenyeji bila sababu za kimisingi.
PAUL KATANA AITAKA TUME YA POLISI NCHINI KUWAHAMISHA BAADHI YA MAAFISA WA POLISI WALIOHUDUMU KWA MIAKA MINGI ENEO LA KALOLENI

