HIMIZO LATOLEWA KWA WENYEJI WA GANDA KAUNTI YA KILIFI KUTAFUTA MAENEO MAALUMU YA MIRADI YA SERIKALI KUTEKELEZWA

Naibu chifu wa eneo la Ganda kaunti ya Kilifi Ann Ziro amewahimiza wenyeji kutafuta maeneo maalum na ya yaliyosalama kwa miradi ya umma ambayo inapendekezwa kutekelezwa na serikali.

Ann Ziro amesema ni kupitia hatua hiyo ambapo miradi hiyo inatekelezwa kwa haraka ili kuwanufaisha wenyeji wa eneo hilo.

Akizungumza katika eneo hilo la Ganda kwenye kikao na wenyeji hao, Ann Ziro amesema miradi ambayo ilikuwa imependekezwa hapo awali imekuwa yenye manufaa kwa wenyeji wa Ganda.