Shirikisho la soka Fifa limemtuwa refa wa Kenya Mary Njoroge kuwa mwamuzi katika mashindano yajayo ya kombe la dunia.
Mashindano ya kombe la dunia mwaka huu yataandaliwa na mataifa ya Astralia pamoja na New Zealand mwezi july tarehe 20 hadi mwezi agosti tarehe 20.
Mary Njoroge sasa ataungana na marefa 33 pamoja na wasaidizi 55 wakiwemo waamuzi wengine 19 wa kitengo cha VAR.
Haya yatakuwa mashindano yake ya pili kuwa mwamuzi katika anga za kimataifa baada ya kuhusishwa katika mashindano ya mwaka 2019 nchini Ufaransa.

