NIMEKUJA NA ‘SUGUNYO’ , WANYONYI ATAKUTANA NAYO JUMAMOSI – MANDONGA

Bondia maarufu kutoka nchini Tanzania Karim Mandonga amehakikishia mashabiki wake kwamba atapata ushindi katika pambano litakalofanyika wikendi ijayo katika ukumbi wa KICC mjini Nairobi.

Akizungumza na wanahabari mjini Nairobi Mandonga amesema kwamba anafuraha sana kufika nchini Kenya na kupokelewa na mashabiki wake ambao amewaahidi kuwa atamtandika bondia wa kenya Daniel Wanyonyi kwenye mpambano utakaofanyika siku ya jumamosi.

Mandonga hii leo anatarajiwa kufanya ziara katika sehemu mbalimbali mjini Nairobi pamoja na kutembelea maskani kwa mpinzani wake Daniel wanyonyi mitaa ya Gikombaa.

Kesho atashiriki katika zoezi la kupima uzani pamoja na mpinzani wake kabla ya kushuka ulingoni siku ya jumamosi.

Pamoja na hayo, Mandonga amemuahidi Rais William Ruto kwamba analenga kuleta burudani la fani hiyo hapa nchini atakaposhuka ulingoni na ngumi yake mpya kwa jina Sugunyo.