Ipo haja ya viongozi waliochaguliwa kuwakilisha sehemu mbalimbali katika mkoa huu wa pwani kuingilia kati michezo mashinani ili kuokoa vipaji ambavyo huenda vikawa manufaa kwa jamii katika siku za usoni.
Hii ni kulingana na Peter Mole mkufunzi mkuu wa Beach Bay ambayo inashiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa na amekariri kwamba ukata wa kifedha ndio jambo ambalo linakatisha tamaa wachezaji mashinani kuendelea kunoa talanta zao.
Ameeleza kwamba wachezaji hupitia changamoto hasaa za chakula na usafiri wanapokwenda mazoezini lakini pia mechi hivyo kuomba viongozi kupiga jeki vilabu hivi ili kuwawezesha wachezaji hao.

