Mkufunzi Mkuu wa Kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Kenya wanamvinyo Tusker FC Robert Matano amesema anaamini bado watafanya vizuri licha ya kupoteza mchezo wao wa kwanza wa msimu.
Mwalimu Matano amezungumza hayo baada ya vijana wake kukutana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa vijana wa pwani Bandari FC ambapo amesema wataendelea kusalia kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wao kwenye ligi.
Kwenye mechi hiyo, Umaru Kasumba na Andrew Juma walifunga upande wa Bandari na Jackson Macharia alifunga bao la kufutia machozi kwa upande wa Tusker FC.

