Idadi kubwa ya wakaazi wa wadi ya ADU eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi, wanaendelea kupitia changamoto kuu katika kutafuta matibabu ya dharura katika taasisi za afya zilizoko mbali na eneo hilo, kutokana na ukosefu Ambulensi.
Haya ni kwa mujibu wa mwakailishi wadi hiyo Samson Zia, ambaye amesema baadhi ya wale wanaoumwa na nyoka katika eneo la Adu na Kamale, wengi wao huaga kuaga dunia kutokana na changamoto za kutafuta huduma za usafiri hadi mjini Malindi ili kutibiwa.
Akizungumza na wanahabari ameeleza kuwa tayari amefanya mazungumzo na msimamizi mkuu wa idara ya afya katika eneo bunge hilo na kumtaka kutafuta mbinu za kuhakikisha wakaazi wa eneo hilo wanapata huduma za Ambulensi.
Kauli hiyo imeungwa mkono na mwenyekiti wa kamati ya mipango katika eneo hilo Stanley Kombe na pia kusema kuna haja ya serikali ya kaunti ya Kilifi kuipandisha hadhi kituo cha afya cha ADU.
UKOSEFU WA AMBULENSI WAZIDI KUWAATHIRI WENYEJI WA WADI YA ADU

