LIGI YA RABAI KUANZA RASMI MWISHONI MWA JANUARI 2023

Ligi ya FKF eneo bunge la Rabai kaunti ya kilifi  huenda ikaanza rasmi mwishoni mwa mwezi huu wa januari. Hii ni kulingana na katibu wa soka tawi la eneo bunge hilo John Barisa wakati akizungumza na tama la  spoti mchana wa leo kupitia nja ya simu.

Ameeleza kwamba msimu ujao wa mwaka 2022/2023 umevutia vilabu vingi kutoka mashinani na sasa usajili unaendelea wakati ambapo pia wanasubiri ligi za kaunti zianze.

Hata hivyo ukata wa kifedha bado unasalia kuwa changamoto kuu kwa vilabu vya rabai jambo ambalo linafanya vilabu vingine kujitoa katika katika mashindano kutokana na ukosefu wa hela za kugharamikia mechi zao.

Amewataka viongozi wa vilabu vya mashinani  kusimama na vilabu vyao sawia tu wanasiasa waliochaguliwa  kusimama na ahadi walizotoa kwa wanamichezo kipindi cha uchaguzi mkuu uliopita.