SERIKALI YA KAUNTI YA LAMU YATAKIWA KUWEKA MIKAKATI YA KUWEZESHA WENYEJI WA WADI KUPATA MAJI SAFI YA KUNYWA

Himizo limetolewa kwa serikali ya kaunti ya Lamu kuweka mikakati ambayo itawawezesha wenyeji wa Wadi ya Kiunga kupata maji safi ya kunywa.
Kulingana na Naibu kamishna wa eneo hilo la Kiunga Kennedy Mrima wenyeji wa eneo hilo wanakabiliwa na uhaba wa maji.
Amesema ukosefu wa Mvua katika eneo hilo kumechangia kwa wenyeji kukabiliwa na hali hiyo.
Ni hali ambayo amesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa huenda wenyeji wakaendelea kuhangaika hata zaidi.