OMANYALA AFUZU KATIKA IDARA YA POLISI

Mtimkaji mwenye kasi zaidi barani Afrika Ferdinand Omanyala ni kati ya makonstebo 2881 waliofuzu hii leo katika chuo cha mafunzo ya polisi Kiganjo.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na rais William Ruto Omanyala sasa ni kati ya maafande wa Kenya ambao  wamepokea mafunzo ya kutosha kwa huduma kwa umma pamoja na ujuzi  mbali mbali wa kutumikia wakenya.

Ikumbukwe kwamba Omanyala alijitolea kuhudumia idara ya polisi mwaka 2021 pamoja na yeye kuchaguliwa kuwa inspekta.