Aliyekuwa Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Roberto Martinez ametangazwa rasmi kama mkufunzi mpya wa timu ya taifa la Ureno kwenye mkataba utakao mruhusu mkufunzi huyo kuwa katika timu hiyo hadi mwaka 2026.
Martinez alijiuzulu rasmi kutoka ukocha wa timu ya taifa ya ubelgiji baada ya kuwa na matokeo mabaya kwenye kombe la dunia nchini Qatar mwaka jana.
Mkufunzi huyo amekuwa akiongoza Ubegiji kwa kipindi cha miaka sita na kuisaidia timu hiyo kukomaa katika nafasi ya kwanza katika viwango vya fifa kwa kipindi cha miaka mitatu.
Taifa la Ureno lilimfuta kazi Fernando Santos ambaye alikuwa kiongozi tangu mwaka 2014, ambaye alishinda kombe la Euro za mwaka 2016 pamoja na kombe la mataifa bara ulaya mwaka 2019.

